Swali: Kama unavojua hivi sasa tuko wakati wa majira ya baridi. Baadhi ya nyakati hufuta juu ya viatu na si soksi. Huvua viatu nikaswali kisha baadaye nikavivaa. Je, kitendo changu hichi ni sahihi?

Jibu: Ukifuta juu ya kitu basi unatakiwa kukiendeleza. Ni mamoja kitu hicho ni kiatu au soksi. Ukikivua na mguu ukawa peku basi wudhuu´ unachenguka. Kwa sababu ufutaji unasihi kwa kule kubaki kwa kile kilichofutwa juu yake. Kikiondoshwa kitu hicho kilichofutwa mguu unakuwa wazi ambao unalazimika kuoshwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 45
  • Imechapishwa: 29/05/2021