Shaka ya kusoma Tashahhud baada ya kumaliza swalah

Mwanafunzi: Mtu mmoja aliswali kama maamuma, lakini akashtuka pale ambapo imamu alitoa salamu ambapo naye akatoa salamu pamoja naye. Anasema hajui kama alisoma Tashahhud au hapana.

Ibn Baaz: Hii ni shaka baada ya kutoa salamu au ni shaka kabla ya kutoa salamu?

Mwanafunzi: Anasema kuwa hakuhisi isipokuwa alipotoa salamu pamoja na imamu, lakini hajui kama alisoma Tashahhud au hapana.

Ibn Baaz: Kwa maana ya kwamba shaka yake ni baada ya kutoa salamu?

Mwanafunzi: Anasema kuwa hakushtuka isipokuwa pale alipotoa salamu pamoja na imamu?

Ibn Baaz: Akitia shaka baada ya kutoa salamu, basi hakuna kitu juu yake. Msingi ni kwamba amesoma.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1117/من-شك-في-عدم-قراءة-التشهد-وهو-ماموم
  • Imechapishwa: 25/01/2026