Shaafi´iy, Ahmad na Maalik juu ya anayewalingania watu katika Bid´ah

Kutokana na haya – aliyoyasema Imaam al-Aajurriy – madhehebu ya Ahmad, ash-Shaafi´iy na Maalik (Rahimahumu Allaah) wanaonelea ya kwamba yule anayelingania katika Bid´ah anatakiwa kunasihiwa. La sivyo akikataa auawe. Huyu ni mwenye shari zaidi kuliko wakataji njia waharibifu. Wenye kukata njia wanawaharibia watu au baadhi ya watu dunia yao. Ama watu hawa – wanaolingania watu katika Bid´ah – wanawaharibia watu I´tiqaad yao na khaswa leo ambapo Ahl-ul-Bid´ah wanawaenezea watu upotevu kupitia njia za mawasiliano; Intaneti, TV, suhuf, magazeti, vitabu na kadhadlika. Shari yao ni kubwa na kubwa. Lakini hili hata hivyo halihusiani na Bid´ah zote.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26899
  • Imechapishwa: 20/05/2015