Swali: Mtu huyu anauliza kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh.

Jibu: Jamaa´at-ut-Tabliygh ni kundi linalojulikana kuwa ni kundi potevu. Kumeulizwa maswali mengi juu yao na ameyajibu Shaykh Ibn Baaz. Shaykh at-Tuwayjiriy na Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy vilevile wameandika juu yao kama jinsi waandishi wengi pia wameandika juu yao miongoni mwa walio waarabu na wasiokuwa waarabu. Upotevu wao uko wazi kama jua. Hakuna anayewatetea isipokuwa ni mpotevu kama wao. Hakuna mwenye kuwatetea na kuwasapoti na kuwatia katika Ahl-us-Sunnah isipokuwa ni mpotevu. Fahamuni hili. Tahadharini na tahadharisheni [watu] nao. Ni katika Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal. Wana Twuruuq as-Suufiyyah. Pote hili lina [I´tiqaad ya] Huluul, Wahdat-ul-Wujuud, Shirki, Bid´ah, upotevu na ukhurafi…

Hakuna anayewafuata isipokuwa ni mpotevu tu kama jinsi hakuna anayewatetea vilevile isipokuwa ni mpotevu pia.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26895
  • Imechapishwa: 20/05/2015