Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah anasema kila mtu wa Bid´ah ni muongo. Mtu wa Bid´ah ni lazima aseme uongo. Hata kama atasalimika na kuwasemea watu uongo anamsemea uongo Allaah kwa kuingiza Bid´ah katika Dini Yake na kuiasisi na kuinasibisha katika Dini ya Allaah na Shari´ah Yake.

Leo wananasibisha Bid´ah katika Manhaj ya Salaf – tunaomba kinga kwa Allaah.

Manhaj ya Salaf ndio Dini ya Allaah ya haki. Kunasibisha Bid´ah katika Dini ya Allaah, pasina kujali ni Bid´ah gani, ni kumsemea uongo Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26899
  • Imechapishwa: 20/05/2015