Swali: Je, ni sahihi ya kwamba Allaah (Ta´ala) amelingana juu ya ´Arshi kwa dhati Yake na Yeye yuko pamoja nasi kwa Dhati Yake?

Jibu: Allaah (Ta´ala) Yuo juu ya ´Arshi Yake na Yuko pamoja nasi kwa ujuzi Wake na uoni Wake na si kwa dhati Yake. Ametakasika Allaah na hilo utakaso ulio mkubwa. Huu ni msemo wa Ahl-ul-Huluul. Salaf wamewafanyia Takfiyr. Allaah Yuko juu ya ´Arshi Yake na Yuko pamoja nasi kwa ujuzi Wake, usikizi Wake, uoni Wake na Uchungaji Wake. Hafichikani na kitu chochote chenye kujificha.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26900
  • Imechapishwa: 20/05/2015