Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa Allaah yuko pamoja nasi kwa dhati Yake kunakolingana na utukufu Wake?

Jibu: Hili ni kosa. Bali kama walivosema Salaf, upamoja wa ujuzi. Dhati Yake (Subhaanahu wa Ta´ala) iko juu ya ´Arshi.

Swali: Kuna yeyote katika Salaf aliyesema hivo?

Jibu: Simjui yeyote aliyesema hivo. Anayesema hivo atakememewa. Kunapelekea kuchanganyika na viumbe – ametakasika kutokana na hilo. Yuko pamoja na viumbe Wake kwa ujuzi na kuwaona. Haifai kusema kuwa yuko pamoja nao kwa dhati Yake. Yuko juu ya ´Arshi, pamoja na viumbe Wake kwa ujuzi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat ´alaal-Fatwaa al-Hamawiyyah al-Kubraa, uk. 204
  • Imechapishwa: 23/02/2023