Swali: Kuna maasi ambayo hukithiri kutoka kwa watu wengi wakati wa Udhhiyah ambapo wanachukua picha kichinjwa na huku wanadai kuwa picha hizo ni kwa ajili ya kumbukumbu. Unawanasihi nini?

Jibu: Hili ndio mara ya kwanza nalisikia kwamba watu wanapiga picha wakati wa kuchinja kwa ajili ya kumbukumbu. Ni kumbukumbu gani unatakiwa kuwa nayo kwa ajili ya kichinjwa hichi? Watu wote huchinja na kila mmoja anajua namna ya kuchinja. Pasi na shaka yoyote haijuzu kwa mtu kuchukua picha kwa ajili ya kumbukumbu. Kwa sababu picha kwa ajili ya kumbukumbu ni haramu. Picha kwa ajili ya kumbukumbu ni haramu kwa kila hali, ni mamoja kwa njia ya kuchora na mkono, kwa njia ya mfumo wa kamera wa papohapo au mfumo wa kamera ambapo picha ikatolewa baadaye – zote hizo ni haramu. Kwa sababu kuhifadhi picha ni haramu kwa hali yoyote ile isipokuwa zile ambazo dharurah imepelekea kufanya hivo kama mfano wa picha kwa ajili ya kitambulisho, picha zilizo katika pesa, leseni na vyenginevyo ambavo mtu hawezi kujitosheleza navyo. Ni lazima kwa yule ambaye ana picha za kumbukumbu kuzichoma moto. Asiyefanya hivo anapata dhambi. Khaswakhaswa yale yanayofanywa na baadhi ya watu ambapo wanahifadhi picha za vitambulisho vya babu zao, ami zao na wajomba zao – kwa ajili ya kuwakumbuka. Kitendo hicho ni haramu na kinapelekea moyo kufungamana na yule maiti na pengine hata kikapelekea katika kuitia dosari ´Aqiydah.

Kwa kufupiza ni kwamba ni lazima kwa yule ambaye anazo picha kwa ajili ya kumbukumbu azichome moto. Kuhusu zile picha ambazo haja imepelekea kufanya hivo ni zenye kupewa udhuru kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ

“Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika dini.”[1]

Kujengea juu ya haya haijuzu kwa mtu kujichukua picha wakati wa kuchinja kwa sababu ya kuhifadhi picha hizo kwa ajili ya kumbukumbu. Ikiwa haijuzu kuzibakiza kwa ajili ya kumbukumbu, basi picha kwa mfumo huu wa kamera  inakuwa ni upuuzi na kitu kisichokuwa na faida yoyote.

[1] 22:78

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=dhx9SbkYHhc&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 01/01/2021