Selfie kwenye Ka´bah au ´ibaadah nyingine

Swali: Baadhi ya ambao wanajinasibisha na ulingano wanawaomba wengine wawarekodi video wakati amesimama karibu na Ka´bah au katika ´ibaabah nyingine. Je, kitendo hicho ni katika ulingano wenye hekima kwa sababu baadhi yao wanaona kuwa kufanya hivo kuna hekima na kwamba kuchukua video kunawahimiza wengine kuja katika ´Umrah na mfano wake?

Jibu: Sijuzishi picha pasi na dharurah. Picha bila ya dharurah hazijuzu. Picha zinazofaa ni kwa ajili ya vitambulisho, pasipoti, cheti cha daktari na mfano wake. Mengineyo lengo zuri halihalalishi njia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha na akasema kuwa ndio watu watakaokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah[1].

[1] al-Bukhaariy (5954) na Muslim (2107).

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://darulhadith.com/selfie-vid-kabah-och-annan-dyrkan/
  • Imechapishwa: 31/08/2023