Tofauti ya wanachuoni wakati wanapokuwa ni wenye kuegemea dalili na zikatofautiana fahamu na mitazamo yao, wanakuwa ni wenye kupewa udhuru kwa tofauti kama hii. Lakini hata hivyo isisemwe kuwa Salaf wametofautiana [katika ´Aqiydah] isipokuwa watapopinga kuwepo kwa kalamu, ikiwa baadhi yao wanapinga kuwepo kwake na wengine hawaitambui uwepo wake. Hii ndio tofauti ya ki-´Aqiydah. Mfano wa hilo pia ni kusema kwamba ´Arshi imeumbwa au haikuumbwa. Kwa kuwa msisahau kuko baadhi ya watu ambao wanakanusha ´Arshi. Miongoni mwa hao ni Sayyid Qutwub anatilia shaka juu yake na kusema hatujui ni nini ´Arshi. Tunamuomba Allaah afya.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/384)
  • Imechapishwa: 26/08/2020