Mama wa waumini Sawdah bint Zam´ah bin Qays al-Qurashiyyah al-´Aamiriyyah.

Yeye ndiye mwanamke wa kwanza aliyeolewa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya Khadiyjah[1]. Aliikaa naye miaka mitatu, kama si zaidi, kabla ya kumuoa ´Aaishah[2].

Alikuwa ni mwanamke mtukufu na mbora na mwerevu.

Mara ya kwanza alikuwa ameolewa na as-Sakran bin ´Amr, kaka yake na Suhayl bin ´Amr al-´Aamiriy.

Yeye ndiye mwanamke ambaye alijitolea siku yake kwa ajili ya ´Aaishah kwa ajili ya kujali moyo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[3]. Kipindi hicho alikuwa ameshakuwa mtumzima.

Amesimulia Hadiyth na al-Bukhaariy amehadithia kutoka kwake.

Ibn ´Abbaas amehadithia kutoka kwake na Yahyaa bin ´Abdillaah al-Answaariy.

Alikufa mwishoni mwa ukhaliyfah wa ´Umar.

´Aaishah amesema:

“Hakuna mwanamke ambaye nilitamani kuwa na ngozi yake kama Sawdah bint Zam´ah ambaye alikuwa ni mwanamke mwenye bidii[4].”[5]

Ibn Sa´d amesema:

“Sawdah na mume wake walisimuli na wakahajiri kwenda Uhabeshi.”

Sawdah amesema:

“Ee Mtume wa Allaah! Jana jioni niliswali nyuma yako. Wakati ulipoenda katika Rukuu´, nikajizuia kwenye pua kwa kuogopa damu isije kutoka. Akaanza kucheka.” Nyakati fulani alikuwa akimchekesha.”[6]

Swaalih, mtumwa aliyeachwa huru na at-Taw´amah, amesimulia kwamba Abu Hurayrah amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika hijjah ya kuaga:

“[Hijjah] hii. Kisha baadaye itakuwa ni kulazimiana na nyumba zenu.”

Swaalih amesema:

Baada ya hapo Sawdah alikuwa anasema: “Sintohiji tena baada yake.”[7]

Ibn Siyriyn amesema:

“´Umar alimtumia Sawdah mkoba wa dirhamu. Akasema: “Hiki ni kitu gani?” Wakasema: “Dirhamu.” Akasema: “Ndani ya mkoba kuna kitu kinacholingana na tende. Nipeni chombo. Kisha akazigawanya.”

Sawdah amepokea Hadiyth tano. Miongoni mwa Hadiyth hizo kuna ambazo ziko kwa al-Bukhaariy na Muslim, al-Bukhaariy amepokea Hadiyth moja.

[1] an-Nawawiy amesema:

”Ibn ´Abdil-Barr amesema: ”Haya ndio maoni ya Qataadah na Abu ´Ubaydah.” Maoni hayohayo yako na Muhammad bin Ishaaq, Muhammad bin Sa´d, Ibn Qutaybah na wengineo.” (Sharh Swahiyh Muslim (10/42))

[2] Ibn Hajar amesema:

”Alimuoa Sawdah Makkah wakati ´Aaishah alipokuwa na miaka sita.” (al-Iswaabah fiy Tamyiyz-is-Swahaabah (4/338))

[3] an-Nawawiy amesema:

”Hapa kuna dalili kwamba inafaa kwa mwanamke kupeana siku yake kwa mke mwingine wa mume kwa sababu ni haki yake. Hata hivyo imeshurutishwa mume akubali kwa sababu ana haki ya kustarehe na mke ambaye kajitolea siku yake. Haifai akachukua kitu mbadala kwa ajili ya siku aliyojitolea. Lakini anaweza kumpa yule amtakaye… Mwanamke ambaye amejitolea siku yake anaweza kuichukua tena pale anapotaka.” (Sharh Swahiyh Muslim (10/42))

[4] al-Qaadhwiy ´Iyaadhw al-Maalikiy amesema:

“Hakusudii kumkosoa kwa sababu hakuwa na nia ya kumdharau.” (Ikmaal-ul-Mu´lim (4/666))

an-Nawawiy amesema:

“Makusudio ni kumsifu kwa moyo wenye nguvu na maumbile mazuri.” (Sharh Swahiyh Muslim ((10/43))

[5] Muslim (1463).

[6] at-Twabaqaat al-Kubraa (8/269).

[7] Ahmad (2/446).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (2/265-269)
  • Imechapishwa: 07/10/2020