72- Haijuzu kuliswalia jeneza kati ya makaburi. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) aliyeeleza:

“Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuliswalia jeneza kati ya makaburi.”

Ameipokea Ibn-ul-A´raabiy katika “al-Mu´jam” yake (Makhtuta 01/235), at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw” (02/80/01) na adh-Dhwiyaa´ al-Maqdisiy amepokea kupitia njia yake katika “al-Ahaadiyth al-Mukhtaarah” (02/79- Musnad ya Anas). al-Haythamiy amesema katika “al-Mu´jam” (03/36):

“Cheni ya wapokezi wake ni nzuri.”

Hadiyth ina njia nyingine kutoka kwa Anas kwa adh-Dhwiyaa´ ambapo Hadiyth inapata nguvu kwayo.

Ameipokea pia Abu Bakr bin Abiy Shaybah katika “al-Muswannaf” (02/185), Abu Bakr bin al-Athram kama ilivyotajwa katika “Fath-ul-Baariy” ya al-Haafidhw Ibn Rajab al-Hanbaliy (01/81/65 al-Kawaakib) kutoka kwa Anas:

“Ilikuwa ikichukizwa kujenga msikiti kati ya makaburi.”

Wapokezi wake ni waaminifu na ni wapokezi wa al-Bukhaariy na Muslim.

Vilevile Hadiyth inashuhudiwa na yale yaliyopokelewa kwa njia nyingi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya makatazo ya kuyafanya makaburi ni mahala pa kuswalia. Nimetaja yaliyopokelewa juu ya hilo mwanzoni mwa kitabu changu “Tahdhiyr-us-Saajid min ittikhaadh-il-Qubuur Masaajid”. Nitataja baadhi yake katika masuala ya 128 nambari. 09.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 138-139
  • Imechapishwa: 07/10/2020