Swali: Vipi tutawaradi baadhi ya ndugu wa Jamaa´at-ut-Tabliygh? Kwa kuwa wanatumia hoja kwa baadhi ya wanachuoni kuwasifia. Pamoja na kujua, mwenye kuwasifia anafikiria matendo yao mengi yanayokwenda kinyume na Uongofu wa Salaf?
Ni ipi Radd yako kwa mwenye kusema hatuhitajii kusema “Salafiy”, “Ikhwaaniy” au “Tabliyghiy”, bali sisi sote ni ndugu wenye kupendana na wenye kusaidizana.
Jibu: Mashaa Allaah. Mashaa Allaah. Huyu ni mshirikina na huyu ni mpwekeshaji, tuwafanye kuwa kitu kimoja? Tunaomba kinga kwa Allaah. Huyu ni Sunniy na huyu ni Mubtadiy´, tuwafanye kuwa kitu kimoja? Tunaomba kinga kwa Allaah. Ni maneno gani haya?! Vipi twaweza kupendana? Tunapendana na kusaidizana katika haki au batili?
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ
“Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari” (03:11)
Iko wapi kuamrishana mema na kukatazana munkari ikiwa atapendwa mshirikina na kupendwa mtu wa Bid´ah? Yako wapi haya? Iko wapi al-Walaa´ wal-Baraa´? Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema:
لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ
“Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao amewaandikia katika nyoyo zao imani na akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake” (57:22)
Yako wapi haya? Kupenda na kuchukia, al-Walaa´ wal-Baraa´, lazima yapatikane kwa muislamu wa kweli, la sivyo Imani yake ni dhaifu.
- Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=35571
- Imechapishwa: 03/09/2020

Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=35571
Imechapishwa: 03/09/2020
https://firqatunnajia.com/salafiy-ikhwaaniy-tabliyghiy-sote-ni-ndugu-tupendane/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)