Swali: Ni ipi hukumu ya mazulia mekundu Msikitini na ni ipi hukumu ya kufanya khuruuj na Jamaa´at-ut-Tabliygh, ambao wanaitwa “wapendwa”?

Jibu: Mazulia yote ambayo ni mazuri yanajuzu. Hakutazamwi rangi sawa ikiwa nyekundu au nyingine. Muhimu ni kwamba mazulia yawe mazuri kwa wenye kuswali.

Ama kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh, sisi tumeshikamana na njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake. Yale ambayo yanaafikiana na njia ya Mtume, Maswahabah wake na Salaf-us-Swaalih, tunayafuata. Yale yanayokwenda kinyume na hayo, tunajitenga nayo.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katutahadharisha na Bid´ah na mapote yanayokwenda kinyume na yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sisi tuko katika mfumo ya wazi na himidi zote ni za Allaah. Tusilete mifumo na njia kutoka kwa wengine. Sisi tuko katika Manhaj ya wazi. Kwa nini tuache Manhaj hii na kwenda kwenye zingine:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate vijia vitakufarikisheni na njia Yake.” (06:153)

Sisi hatuna haja ya mifumo hii au njia hizi. Hatuihitajii. Allaah katuneemesha Uislamu na katuamrisha kushikamana na njia iliyonyooka. Allaah haridhii kutoka kwetu isipokuwa kufuata njia aliyotuwekea. Yale yanayoafikiana nayo ndio ya haki na yale yanayokwenda kinyume nayo ni yenye kurudishwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: www.alfawzan.af.org.sa/node/13537
  • Imechapishwa: 03/09/2020