Ibn Baaz akisifia Jamaa´at-ut-Tabliygh na al-Ikhwaan al-Muslimuun kabla ya kufa kwake?

Swali: Wamedhihiri baadhi ya Madu´aat wanaosema ya kwamba Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) kafariki naye anasifia na kunasihi watu na Jamaa´at-ut-Tabliygh na al-Ikhwaan al-Muslimuun. Maneno haya ni kweli?

Jibu: Maneno haya si sahihi. Na sisi tulikaa nae zaidi ya miaka kumi hatukumsikia akisifia isipokuwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, na akilingania katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Na akinasihi waliokosea katika makundi mengine warejee makosa yao, Tabliyghiyyuun na mengine. Haya ndio nijuayo kwa Shaykh wangu, Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133663
  • Imechapishwa: 03/09/2020