Swali: Baadhi ya ndugu katika mji wangu wanawatukana watu wasiofuata mfumo wa Salaf, wanataja sifa zao mbaya na wanasema kuwa watu hawa hawana heshima yoyote na inajuzu kuwasengenya. Je, ni sahihi?

Jibu: Hapana, sio sahihi. Je, ni katika mfumo wa Salaf-us-Swaalih kuwatukana na kuwajeruhi watu na kuwadharau wenye kwenda kinyume? Hili sio katika mfumo wa Salaf-us-Swaalih. Nimeshawaambieni: ambaye anajinasibisha na mfumo wa Salaf ni lazima asome mfumo wao na awajue. Haitoshelezi kujinasibisha na wao tu. Salaf hawakuwa wakijeruhi, kutukana na kusengenya watu. Hawakuwa wakifanya hivi. Wananasihi bila ya kufedhehesha. Nasaha sio fedheha. Huu ndio mfumo wa Salaf-us-Swaalih.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mqirwani–14340317.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015