Swali: Familia yangu inajinasibisha na pote la ki-Suufiy Tijaaniyyah. Wanasherehekea kuzaliwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanafanya Bid´ah nyingi. Wanasema kuwa hatumpendi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio maana hatusherehekei maulidi na wao ndio wenye kumpenda (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vipi mtu atajibia hili?

Jibu: Mwambie wale wenye kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanamfuata. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutuwekea kusherehekea maulidi katika Shari´ah. Si yeye wala Maswahabah zake hawakufanya. Ikiwa kweli unampenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi usifanye maulidi. Mtume amekataza Bid´ah na hili ni katika Bid´ah. Nenda nao kwa kuwafupishia njia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mqirwani–14340317.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015