Swali: Ni kwa nini tunasoam vitabu vya Fiqh wakati vitabu vya Hadiyth vinatosheleza? Ukiongezea juu ya hilo ni kwamba maimamu wamekataza kujishughulisha na maneno yao badala ya Sunnah?

Jibu: Fiqh ni maana ya Sunnah. Fiqh ni maana zilizotolewa kwenye Hadiyth. Fiqh haikutolewa kwenye falsafa, wanafalsafa au fikira za watu. Imechukuliwa kutoka kwenye Hadiyth. Hata hivyo kunaweza kutokea kosa katika uelewa, ufahamu au maoni. Lakini kwa jumla madhehebu mane ni katika madhehebu ya Salaf. Ni wanafunzi wa Salaf.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mqirwani–14340317.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015