1- Twaawuus amesema:

“Nafsi ya kijana haikamiliki mpaka aoe.”

2- Ibraahiym bin Maysarah amesema:

“Twaawuus alinambia: “Oa.” Vinginevyo nitakwambia yale ambayo ´Umar bin al-Khattwaab alisema kumwambia Abuz-Zawaaid: “Hakuna kinachokukosesha kuoa isipokuwa kushindwa au maovu.”[1]

3- Ibn Buraydah amesema:

“Mtu anapaswa kuhakikisha ameacha mambo matatu: Kutembea; akihitaji kufanya hivo basi anaweza kutembea. Asiache chakula, matumbo yake yatabana. Asiache kufanya jimaa; kwani hakika kisima kisipotumiwa basi maji yake hukauka.”[2]

Anatakiwa kuyafanya mambo haya kwa uwastani na khaswa jimaa. Atapokuwa mzee bora ni yeye kuacha kufanya jimaa.

4- al-Qaasim bin Muhammad amesema:

“´Aaishah alikuwa peke yake katika kutoa fatwa katika zama za Abu Bakr na ´Umar mpaka alipofariki. Nilikuwa ni mwenye kulazimiana naye licha ya kuwa nilikuwa naweza kusema mambo yasiyokuwa na maana.”[3]

5- Maymuun bin Mihraan amesema:

“Usipewe majaribio kwa mambo matatu: Usimwendee mtawala ingawa utainong´oneza nafsi yako kwamba utamwamrisha kumtii Allaah. Usisikilize uzushi wowote; kwani hakika hujui ni kipi kitachofungamana na moyo wako. Usiingie kwa mwanamke ingawa utainong´oneza nafsi yako kwamba utamfunza Kitabu cha Allaah.”[4]

6- Maymuun bin Mihraan amesema:

“Napendelea zaidi kushika jukumu la kusimamia hazina ilio na pesa kuliko kumsimamia mwanamke.”[5]

7- Abul-Maliyh amesema:

“Alikuja bwana mmoja kwa Maymuun bin Mihraan kumchimbia msichana wake. Maymuun akasema: “Si mzuri kwako.” Bwana yule akasema: “Kwa nini?” Akasema: “Kwa sababu anapenda kujipamba na kujipodoa.” Bwana yule akasema: “Nina kila anachokitaka.” Maymuun akasema: “Sasa naona kuwa wewe si mzuri kwake.”[6]

8- ´Atwaa´ amesema:

“Lau ningepewa jukumu la kusimamia hazina ilio na pesa basi ningekuwa mwaminifu zaidi. Hata hivyo siiamanishi nafsi yangu juu ya mwanamke mbaya.”

Amesema kweli (Rahimahu Allaah). Imekuja katika Hadiyth:

“Mwanamme asikae faragha na mwanamke, kwa sababu wa tatu wao ni shaytwaan.”[7][8]

9- Saalim na Naafiy´ walitofautiana juu ya Hadiyth tatu zilizopokelewa na Ibn ´Umar. Saalim alikuwa bora kuliko Naafiy´. Lakini Hadiyth tatu hizi za Naafiy´ ndio ambazo ni sahihi zaidi. Tumefikiwa na khabari kwamba siku moja walipitia Hadiyth ya kumwingilia mwanamke kwa nyuma ambayo Naafiy´ amepwekeka nayo katika kuipokea kutoka kwa bwana wake (Ibn ´Umar). Maymuun bin Mihran akasema:

“Naafiy´ aliyasema haya baada ya kuwa mtumzima na kuondokwa na fahamu.”

Wakamweleza Saalim kwamba Naafiy´ amesema hivo ambapo akasema:

“Mtumwa amesema uongo, au amekosea. Alichokuwa anasema Ibn ´Umar ni kwamba mume amwingilie kwa mbele au kwa nyuma kwenye tupu yake ya mbele.”

Hata hivyo kumepokelewa upokezi mwingine kutoka kwake ambao unaharamisha kumwingilia mwanamke kwa nyuma. Ikiwa yamesihi hayo yaliyopokelewa kutoka kwake basi hayako wazi. Hivyo basi itakuwa alichomaanisha kumwingilia kwa nyuma ni kwenye uke wake. Nimetunga kitabu juu ya maudhui haya. Hakuna mwanachuoni anayekisoma isipokuwa anayakinisha kwamba jimaa kwenye tupu ya nyuma ni haramu.

Maneno ya Maymuun bin Mihraan amesema “Naafiy´ aliyasema haya baada ya kuwa mtumzima na kuondokwa na fahamu.” ni maneno nyonge. Bali Ummah umekubaliana kwamba ni hoja ya kukata kabisa.[9]

10- Thaabit al-Bunaaniy amesema:

“´Awn alikuwa na kijakazi akiitwa Bushrah na akisoma kwa sauti nzuri kabisa. Siku moja akamwambia: “Wasomee ndugu zangu.” Akaanza kusoma kwa sauti ya machungu na ya kusitikisha. Nikawaona namna wanavyotupa vilemba vyao na kuanza kulia. Siku moja akamwambia: “Ee Bushrah! Nimekupa dinari 1000 kwa ajili ya uzuri wa sauti yako. Nenda zako. Hakika wewe uko huru kwa ajili ya Allaah.”[10]

[1] 5/48.

[2] 5/52.

[3] 5/55.

[4] 5/77.

[5] 5/77.

[6] 5/75.

[7] Ahmad (1/81) na at-Tirmidhiy (2166).

[8] 5/87-88.

[9] 5/100-101.

[10] 5/105.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’
  • Imechapishwa: 31/12/2020