Maoni tatu tofauti juu ya josho la siku ya ijumaa

Swali: Ni ipi hukumu ya josho la ijumaa?

Jibu: Josho la ijumaa wanachuoni wametofautiana. Kikosi cha wanachuoni wengi wanaona kuwa ni jambo limependekezwa. Hilo ni kutokana na Hadiyth isemayo:

“Ambaye atatawadha siku ya ijumaa ni vyema. Na ambaye ataoga ndio bora zaidi.”

Wanachuoni wengine wakaona kuwa ni jambo la lazima. Wamejengea hoja kwa Hadiyth ya Abu Sa´iyd isemayo:

“Josho la ijumaa ni wajibu kwa kila mwenye kuota.”

Hadiyth hii ni Swahiyh zaidi kuliko yenye kusema:

“Ambaye atatawadha siku ya ijumaa ni vyema… “

Wapo wanachuoni wengine wenye kuona kuwa kuoga ni lazima kwa wale wafanya kazi pasi na wengine. Wamejengea hoja kwa Hadiyth ya ´Aaishah isemayo:

“Watu walikuwa wanakuja siku ya ijumaa ambapo wanatokwa na harufu kwa sababu walikuwa ni wafanya kazi. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaambia:

“Laiti mngelioga.”

Kwa hivyo masuala haya kuna maoni tatu tofauti ya wanachuoni. Jopo la wanachuoni wengi wanaona kuwa imependekezwa na mapendekezo yanakuwa na nguvu zaidi ikiwa mtu ataoga.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 01/01/2021