21- Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid amesema:

“Abu Salamah alitujia kipindi cha Bishr bin Marwaan. Alikuwa amemuoza msichana wake kwa viganja viwili vilivyojazwa tende kama mahari.”[1]

22- Sa´iyd bin Jubayr amesema:

“Nilidonolewa na nge ambapo mama yangu akaapa kwa Allaah kwamba natakiwa nimwombe mtu anifanyie matabano. Nikaenda kwa mfanya matabano na nikampa mkono ambao sio. Sikutaka atoe kafara ya kiapo chake.”[2]

23- adh-Dhahabiy amesema:

“´Aaishah bint Twalhah aliolewa na binamu yake ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Bakr. Baada ya hapo akaolewa na kiongozi wa ´Iraaq Musw´ab ambaye alimpa dinari 100.000 kama mahari. Inasemekana kwamba alikuwa mwanamke mrembo na mwenye busara sana. Hadiyth zake zimetajwa katika vitabu Swahiyh. Alipouliwa Musw´ab bin az-Zubayr aliolewa na ´Umar bin ´Ubaydillaah at-Taymiy ambaye alimpa mahari ya dirhamu 100.000.  Mshairi amesema juu ya hilo:

Msichana apewe 100.000 kamilifu

ilihali wanajeshi mashujaa wanalala njaa[3]

24- ´Abdullaah bin ´Amr amesema:

“Twubay´! Ametuhadithia juu ya mambo matatu.” Amesema: “Ulimi wenye kusema ukweli, moyo wenye kumcha Allaah na mwanamke mwema.”[4]

25- ´Urwah bin az-Zubayr amehadithia kidogo kutoka kwa baba yake kwa sababu ya udogo wake. Amehadithia vilevile kutoka kwa mama yake Asmaa´ bint Abiy Bakr as-Swiddiyq na kutoka mama yake mdogo mama wa waumini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye alilazimiana naye na akachukua elimu yake kwake.”[5]

26- ´Urwah amesema:

“´Aaishah hakufa isipokuwa baada ya kumwacha kwa miaka mitatu.”[6]

27- Shaykh wetu Abul-Hajjaaj ametaja katika kitabu chake “Tahdiyb-ul-Kamaal” baadhi ya waalimu wa ´Urwah:

1- Mama yake Asmaa´.

2- Mamake mdogo ´Aaishah.

3- Asmaa´ bint ´Umays.

4- Umm Habiybah.

5- Umm Salamah.

6- Umm Haaniy´.

7- Umm Shariyk.

8- Faatwimah bint Qays.

9- Dhubaa´ah bint az-Zubayr.

10- Buswrah bint Swafwaan.

11- Zaynab bint Abiy Salamah.

12- ´Amrah al-Answariyyah.[7]

28- Ibn Jurayj amesema:

“Kumsikia Mujaahid na nikasema kuwa nimesikia kutoka kwake ni jambo linalopendeza zaidi kwangu kuliko familia na mali yangu.”[8]

29- Naafiy´ amesema:

“Ibn ´Umar alikuwa akimbusu [mwanae] Saalim na akisema: “Mzee anambusu mzee.””[9]

30- Ibn Abiyz-Zinaad amesema:

“Watu wa al-Madiynah walikuwa wanachukia kuzaa na wajakazi mpaka kwanza wajakazi hao wazae mabwana waheshimiwa kama mfano wa ´Aliy bin al-Husayn, al-Qaasim bin Muhammad na Saalim bin ´Abdillaah. Hawa ndio walikuwa watu bora wa al-Madiynah inapokuja katika elimu, uchaji, ´ibaadah na kujichunga. Baada ya hapo kila mmoja akawa anataka masuria.”[10]

[1] 4/290.

[2] 4/333.

[3] 4/369.

[4] 4/412.

[5] 4/421.

[6] 4/424.

[7] 4/434-435.

[8] 4/451.

[9] 4/460.

[10] 4/460.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’
  • Imechapishwa: 30/12/2020