21- Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid amesema:
“Abu Salamah alitujia kipindi cha Bishr bin Marwaan. Alikuwa amemuoza msichana wake kwa viganja viwili vilivyojazwa tende kama mahari.”[1]
22- Sa´iyd bin Jubayr amesema:
“Nilidonolewa na nge ambapo mama yangu akaapa kwa Allaah kwamba natakiwa nimwombe mtu anifanyie matabano. Nikaenda kwa mfanya matabano na nikampa mkono ambao sio. Sikutaka atoe kafara ya kiapo chake.”[2]
23- adh-Dhahabiy amesema:
“´Aaishah bint Twalhah aliolewa na binamu yake ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Bakr. Baada ya hapo akaolewa na kiongozi wa ´Iraaq Musw´ab ambaye alimpa dinari 100.000 kama mahari. Inasemekana kwamba alikuwa mwanamke mrembo na mwenye busara sana. Hadiyth zake zimetajwa katika vitabu Swahiyh. Alipouliwa Musw´ab bin az-Zubayr aliolewa na ´Umar bin ´Ubaydillaah at-Taymiy ambaye alimpa mahari ya dirhamu 100.000. Mshairi amesema juu ya hilo:
Msichana apewe 100.000 kamilifu
ilihali wanajeshi mashujaa wanalala njaa[3]
24- ´Abdullaah bin ´Amr amesema:
“Twubay´! Ametuhadithia juu ya mambo matatu.” Amesema: “Ulimi wenye kusema ukweli, moyo wenye kumcha Allaah na mwanamke mwema.”[4]
25- ´Urwah bin az-Zubayr amehadithia kidogo kutoka kwa baba yake kwa sababu ya udogo wake. Amehadithia vilevile kutoka kwa mama yake Asmaa´ bint Abiy Bakr as-Swiddiyq na kutoka mama yake mdogo mama wa waumini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye alilazimiana naye na akachukua elimu yake kwake.”[5]
26- ´Urwah amesema:
“´Aaishah hakufa isipokuwa baada ya kumwacha kwa miaka mitatu.”[6]
27- Shaykh wetu Abul-Hajjaaj ametaja katika kitabu chake “Tahdiyb-ul-Kamaal” baadhi ya waalimu wa ´Urwah:
1- Mama yake Asmaa´.
2- Mamake mdogo ´Aaishah.
3- Asmaa´ bint ´Umays.
4- Umm Habiybah.
5- Umm Salamah.
6- Umm Haaniy´.
7- Umm Shariyk.
8- Faatwimah bint Qays.
9- Dhubaa´ah bint az-Zubayr.
10- Buswrah bint Swafwaan.
11- Zaynab bint Abiy Salamah.
12- ´Amrah al-Answariyyah.[7]
28- Ibn Jurayj amesema:
“Kumsikia Mujaahid na nikasema kuwa nimesikia kutoka kwake ni jambo linalopendeza zaidi kwangu kuliko familia na mali yangu.”[8]
29- Naafiy´ amesema:
“Ibn ´Umar alikuwa akimbusu [mwanae] Saalim na akisema: “Mzee anambusu mzee.””[9]
30- Ibn Abiyz-Zinaad amesema:
“Watu wa al-Madiynah walikuwa wanachukia kuzaa na wajakazi mpaka kwanza wajakazi hao wazae mabwana waheshimiwa kama mfano wa ´Aliy bin al-Husayn, al-Qaasim bin Muhammad na Saalim bin ´Abdillaah. Hawa ndio walikuwa watu bora wa al-Madiynah inapokuja katika elimu, uchaji, ´ibaadah na kujichunga. Baada ya hapo kila mmoja akawa anataka masuria.”[10]
[1] 4/290.
[2] 4/333.
[3] 4/369.
[4] 4/412.
[5] 4/421.
[6] 4/424.
[7] 4/434-435.
[8] 4/451.
[9] 4/460.
[10] 4/460.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’
- Imechapishwa: 30/12/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)