Safari kwa ajili ya kwenda kuswali Tarawiyh mji mwingine

Swali: Unasemaje kuhusu kufunga safari kwenda katika mji mwingine ambao sikai ili kuswali na imamu swalah ya Tarawiyh?

Jibu: Hapana neno. Hapana vibaya mtu kufunga safari kwa ajili ya kwenda kuswali na mtu, kumtembelea mgonjwa au kumtembelea kwa ajili ya Allaah na kwa ajili nampenda kwa ajili ya Allaah. Kilichokatazwa ni kufunga safari kwenda maeneo fulani palipo msikiti mbali na ile misikiti mitatu au maeneo mengine yanayotukuzwa. Hiki ndicho kilichokatazwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msifunge safari isipokuwa kuiendea misikiti mitatu; msikiti Mtakatifu, msikiti huu na msikiti wa al-Aqswaa.”

Haifai kufunga safari kuuendea msikiti wowote mwingine isipokuwa hii mitatu peke yake au maeneo yoyote. Hata hivyo hapana vibaya kufunga safari kwenda kumtembelea ndugu yako kwa ajili ya Allaah, kumtembelea mgonjwa au kwa ajili ya biashara.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 30/03/2023