Swali: Inatokea kwa watu wengi wakala siku nyingi za Ramadhaan na wasikumbuke idadi ya siku hizo. Maswali kama hayo yanakariri. Ni ipi hukumu ya kitendo hicho?

Jibu: Ni lazima kwa ambaye ana shaka ajitahidi. Akitilia shaka juu ya siku ajitahidi na atendee kazi lile la salama zaidi. Akitilia shaka kati ya siku tatu au nne afanye ni siku nne, akitilia shaka kati ya siku nne au tano afanye siku tano. Achukue tahadhari kwa ajili ya dini yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 30/03/2023