Swali: Ni yepi masharti ya mapenzi kwa ajili ya Allaah? Ni vipi vigezo vyake? Kipi kinachompasa ndugu ikiwa anampenda ndugu yake?

Jibu: Kupendana kwa ajili ya Allaah ni kwa dhahiri yake; kwamba anampenda kwa sababu ya matendo yake mema. Hayo ndiyo masharti yake, kwa maana kumpenda kwa ajili ya Allaah kutokana na matendo yake mema na uchaji wake kwa Allaah. Hampendi kwa sababu ya dunia, nasaba au ujirani. Anampenda kwa ajili ya Allaah kwa sababu ya matendo yake mema na kunyooka kwake sawa juu ya dini ya Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31341/ما-واجبات-وضوابط-المحبة-في-الله
  • Imechapishwa: 19/10/2025