Je, ni lazima kujitapisha chakula cha haramu alichokula mtu?

Swali: Kitendo cha as-Swiddiyq, mtu anayekula kitu cha haramu kisha akajua baada ya kula, anatakiwa atapike?

Jibu: Akipatwa na kichefuchefu akakitapika ni vizuri. Lakini kama hakufanya hivyo, haimlazimu, kwa sababu huenda ikawa ni jambo gumu kwake. Ni mwenye udhuru kwa kuwa hakujua. Lakini akikitapika kwa kufuata mfano wa as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh), basi ni jambo jema, kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jilazimiani na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31350/هل-يلزم-من-علم-انه-اكل-حراما-ان-يقيىه
  • Imechapishwa: 19/10/2025