Swali: Kumeenea kati ya wanawake kuvaa suruwali zenye kubana zinazobainisha umbo la miguu ya mwanamke kiasi kwamba suruwali hizo huonekana chini ya ´Abaa´ah fupi katika masoko na maeneo ya wazi, jambo linalosababisha fitina kwa wanaume na wauzaji. Ni nasaha gani mnayoitoa?
Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kuvaa kitu kinachosababisha fitina wala kuvaa kitu kinachokwenda kinyume na mavazi ya watu wa nchi yake, kwa kuwa hilo ni vazi la kujionyesha umaarufu, na mavazi ya kujionyesha umaarufu yamekatazwa. Kwa hiyo haifai kwake kuvaa kitu kinachofanana na mavazi ya wanaume, kinachoonyesha baadhi ya sehemu zake za siri au kinachopingana na mavazi ya watu wa nchi yake. Bali inampasa awe kama wanawake wa nchi yake katika mavazi yao, akiwa amejisitiri na kuwa makini kujiepusha na kujifananisha na wanaume, si inapokuja katika suruwali au vinginevyo. Vema avae mavazi ya kawaida yaliyozoeleka katika nchi yake na dada zake kwa ajili ya Allaah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31332/ما-حكم-لبس-البنطلون-الضيق-للنساء
- Imechapishwa: 19/10/2025
Swali: Kumeenea kati ya wanawake kuvaa suruwali zenye kubana zinazobainisha umbo la miguu ya mwanamke kiasi kwamba suruwali hizo huonekana chini ya ´Abaa´ah fupi katika masoko na maeneo ya wazi, jambo linalosababisha fitina kwa wanaume na wauzaji. Ni nasaha gani mnayoitoa?
Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kuvaa kitu kinachosababisha fitina wala kuvaa kitu kinachokwenda kinyume na mavazi ya watu wa nchi yake, kwa kuwa hilo ni vazi la kujionyesha umaarufu, na mavazi ya kujionyesha umaarufu yamekatazwa. Kwa hiyo haifai kwake kuvaa kitu kinachofanana na mavazi ya wanaume, kinachoonyesha baadhi ya sehemu zake za siri au kinachopingana na mavazi ya watu wa nchi yake. Bali inampasa awe kama wanawake wa nchi yake katika mavazi yao, akiwa amejisitiri na kuwa makini kujiepusha na kujifananisha na wanaume, si inapokuja katika suruwali au vinginevyo. Vema avae mavazi ya kawaida yaliyozoeleka katika nchi yake na dada zake kwa ajili ya Allaah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31332/ما-حكم-لبس-البنطلون-الضيق-للنساء
Imechapishwa: 19/10/2025
https://firqatunnajia.com/vaa-mavazi-kama-ya-dada-zako-wengine/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket