Saa zilizotiwa dhahabu kwa wanamme na wanawake

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa saa zilizopakwa dhahabu nyeupe?

Jibu: Saa zilizotiwa dhahabu kwa wanawake zinafaa na ni haramu kwa wanamme. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameharamisha dhahabu kwa wanamme.

Kuhusiana na dhahabu nyeupe, mimi sijui kama kuna dhahabu nyeupe. Dhahabu zote zinakuwa na rangi ya dhahabu. Lakini pengine muulizaji analenga fedha. Fedha haitokani na dhahabu. Inafaa kutumia fedha pale ambapo haifai kutumia dhahabu, kama vile pete na vyenginevo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/108)
  • Imechapishwa: 10/05/2021