Rushwa kwa ajili ya kuthibitisha haki na kutokomeza batili

Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwa ambaye anatoa rushwa ili athibitishe haki na kuitokomeza batili pamoja na kuzingatia kwamba asipotoa rushwa basi itathibitishwa batili – Allaah asijaalie?

Jibu: Allaah (´Azza wa Jall) ameharamisha rushwa na akamlaani mtoa rushwa na mpokeaji kupitia ndimi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Rushwa maana yake ni mtu kutanguliza pesa ili apindishiwe yule mtoaji kutokana na haki na kuiendea batili, ili yule mtoa hongo apewe kisicho haki yake, atangulizwe mbele ya wengine au batili nyingine mfano wa hiyo. Hii ndio rushwa. Haijuzu kumtanguliza yeye mbele ya yeyote. Bali ni katika madhambi makubwa, ni katika kula mali za watu kwa batili na ni miongoni mwa sababu za kuharibika kwa jamii na kupotea kwa haki.

Haijalishi kitu hata kama atadai mwenye nayo kuwa anapata kuithibitisha haki haifai kwake kutanguliza rushwa. Bali ni lazima kujiepusha na jambo hilo na aombe haki kwa njia zilizowekwa katika Shari´ah ambazo Allaah amewawekea waja Wake na akawahalalishia nazo. Ukifunguliwa mlango huu basi kila mmoja atadai kuwa anatafuta haki na kwamba ameitoa kwa ajili ya kutafuta haki yake. Haifai. Rushwa ni mali ya haramu kwa yule mtoaji na yule mpokeaji na yule mfanyakazi.

Ni lazima kwa yule msimamizi ambaye anataka kupewa rushwa amche Allaah na alazimiane na haki. Ikitambulika kuwa hasimamii kazi yake basi ni lazima kwa ambaye anajua jambo hilo atoe ushuhuda dhidi yake kwa kazi yake mbaya ili apewe malipo yake kwa kutia adabu, kufukuzwa kazi na mfano wa hayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4303/حكم-دفع-الرشوة-لاحقاق-الحق-وابطال-الباطل
  • Imechapishwa: 15/06/2022