Matumizi ya wake inatofautiana kutegemea idadi ya watoto?

Swali: Ikiwa mwanamme yuko na wake wengi ambapo mmoja katika wake hawa yuko na watoto wanne na mwingine yuko na watoto sita. Je, anatakiwa kufanya sawa katika matumizi au anaweza kufanya atakavyo?

Jibu: Kila mmoja atapewa matumizi yake yanayolingana naye. Ambaye ana watoto wanne ana haki yake, ambaye ana watoto sita ana haki yake na ambaye ana watoto nane ana haki yake. Kila mmoja atapewa kile kinachonasibiana naye na watoto wake. Hawalingani kutokana na ima wingi au uchache wa watoto.

Kuhusu mke kama mke anatakiwa kutaamiliwa kama anavotaamiliwa yule mke wake mwingine aliye naye. Kwa msemo mwingine anatakiwa kufanya uadilifu kati yao. Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa atamwangalia kila mmoja kutegemea vile zilivyo desturi na familia zao. Lakini maoni haya hayako wazi. Bali kilicho lazima ni yeye kuchunga na kufanya uadilifu kati yao inapokuja katika riziki, mavazi na yanayogawanywa kwa hali yoyote. Ni mamoja ni mmoja katika wasichana wa matajiri na huyo mwingine ni msichana wa masikini. Kwa hivyo ni lazima kufanya uadilifu kati yao. Ni mamoja katika matumizi, mavazi, malazi na yale yanayogawanywa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4311/هل-تختلف-نفقة-الزوجات-حسب-عدد-الاولاد
  • Imechapishwa: 16/06/2022