Swali: Anauliza kuhusu mavazi yenye kubana, sidiria za matiti na rangi nyekundu ya mdomo?

Jibu: Mavazi ya kubana hayajuzu kwa mwanamke kuyavaa isipokuwa kama atakuwa nyumbani kwake na asiwepo zaidi ya mume wake. Hilo ni kwa sababu mavazi ya kubana yanayoonyesha fumo ya mwili ukweli wa mambo ni kwamba yanazingatiwa kuwa ni yenye kusitiri ilihali si yenye kusitiri. Ni yenye kusitiri kwa njia ya kwamba yameficha rangi ya mwili. Lakini si yenye kusitiri kwa njia ya kwamba fomu ya mwili yaonekana. Kitendo hicho kinaingia ndani ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kuna watu aina mbili wa Motoni sijawaona; wanaume walio na bakora kama mkia wa ng´ombe ambazo wanawapiga kwazo watu, na wanawake waliovaa vibaya, uchi, Maaylaat na Mumiylaat. Vichwa vyao ni kama nundu ya ngamia. Hawatoingia Peponi na wala hawatonusa harufu yake. Harufu yake inapatikana umbali wa kadhaa na kadhaa.”

Kisha baada ya hapo akataja wanawake waliovaa na wakati huohuo wako uchi. Mwanamke huyu ambaye amevaa mavazi yenye kubana yanayoonyesha fomu ya mwili ukweli wa mambo ni kwamba amevaa lakini yuko uchi. Hivyo haijuzu kwake kuvaa mavazi kama haya muda wa kuwa hayuko nyumbani ambapo hakuna zaidi ya mume wake.

Kuhusu sidiria hazina neno. Isipokuwa mimi naona kuwa haitakiwi kwa mwanamke kijana ambaye hajaolewa kuivaa. Kwa sababu hapo ndipo ataanza kukuwa hali ya kupenda kuonekana na kujiweka katika mitihani. Hivyo haitakiwi kwake kuivaa. Hakuna neno kwa mwanamke ambaye ni mke wa mtu ambaye anamvalia mume wake. Ni katika kujipamba.

Ama rangi nyekundu ya mdomoni ni katika mambo ambayo kwayo mwanamke hujipamba. Ni kama hina kwenye mikono na kwenginepo. Msingi ni kujuzu. Kama kumepokelewa kitu kinachopelekea katika uharamu Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (16) http://binothaimeen.net/content/6812
  • Imechapishwa: 23/03/2021