Swali: al-Ahdal anasema kuwa Hasan al-Bannaa na Sayyid Qutwub ni maimamu wawili wa Da´wah. Je, ni kweli?

Jibu: Ni kweli. Ni maimamu. Hata hivyo, ni maimamu wa Ahl-ul-Bid’ah. Dalili ya hilo ni jinsi Sayyid Qutwub alivyochukulia wepesi kwa Maswahabah, imani ya kwamba Allaah yuko katika kila kitu na mambo mengine ambayo ndugu Rabiy’ bin Haadiy (Hafidhwahu Allaah) aliyoyataja.

Kuhusu Hasan al-Bannaa, nilikuwa nikifikiria kuwa ni mzuri na ni mwongofu. Hata hivyo, nimeweka maelezo katika kitabu changu “al-Makhraj min al-Fitnah” ya kwamba ilikuwa ni ufahamu wangu kabla ya kujua madhehebu na uhakika wake. Hivi ninaonelea kuwa amepinda na ni mpotevu.

Mimi binafsi ninaonelea kuwa Hasan al-Bannaa ni mpotevu zaidi kuliko Sayyid Qutwub, kwa sababu anataka kujenga madaraja kati ya Ahl-us-Sunnah na Shiy´ah. Alikuwa akisema kuwa Da´wah yake ni “Suufiyyah Salafiyyah”, akiyazunguka makaburi na akiyapapasa.

Makala ndogo ya ndugu yetu Ahmad ash-Shihhiy inatosha kuona al-Ikhwaan al-Muslimuun ni watu gani kuanzia mwanzo wao. Ninamshukuru Allaah kijana wa kimisri – na kadhalika vijana wengi Sudan, Yemen na Saudi Arabia –wameona ukweli. Hawajaona hata mengi. Wengiliona mengi wangelisema “Fiy kwa Da´wah ya al-Ikhwaan al-Muslimuun!”. Hali kadhalika kuhusu ndugu katika nchi za Ghuba. Wengi wanawapiga vita baada ya kuwa na wao.

Uliyosema kabla ni kweli. Ni maimamu wawili wa Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal na sio Ahl-us-Sunanh.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´qiybaat ´alaa Kitaab as-Salafiyyah laysat Madhhaban, uk. 3-4
  • Imechapishwa: 22/04/2015