Swali: Ni yapi maoni yako kuhusu mwenye kuiponda Salafiyyah na kusema kwamba ni Bid´ah?

Jibu: Mwenye kusema kuwa Salafiyyah ni Bid´ah ni Doctor. Anayejulikana kuwa ni Ash´ariy. Vijana wa leo pengine wamesoma kitabu cha Dr. al-Buutwiy. Yeye ndiye ambaye ameandika kitabu kuhusu kwamba Salafiyyah ni Bid´ah. Dr. al-Buutwiy anaamini Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na wakati huo huo anakanusha Salafiyyah. Mgongano!

Huenda mtu huyu ameathirika na Salafiyyuun Shaam. Kuna Salafiyyuun katika mji wake. Inawezekana kuwa ni chuki baina yake na Salafiyyuun ndio imemfanya kutumbukia katika kujigonga huku. La sivyo mgongano huu ni mbaya sana hata kama al-Buutwiy ni Ash´ariy mwenye kupindukia sana.

Anasema katika kitabu chake “Kubraa al-Yaqiyniyyaat” ya kwamba mtu hawezi kusema kuhusu “Mwingi wa Rehema amelingana sawa juu ya ´Arshi Yake” yale aliyosema Imaam Maalik:

“Kulingana sawa kunajulikana. Namna haijulikani. Kuamini hilo ni wajibu. Kuuliza kuhusu hilo ni Bid´ah.”

Anasema kwamba sisi hatuwezi kusema hivi leo kwa sababu tumesoma balagha na lugha na tumefikia maana ya ndani kabisa katika Qur-aan. Kwa msemo mwingine Dr. al-Buutwiy anadai kuwa yeye ni bingwa zaidi wa lugha kuliko Imaam Maalik bin Anas. Kwa ajili hiyo yeye hawezi kushikamana na yale waliyoshikamana nayo Waislamu waliotangulia.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Amaan bin ´Aliy al-Jaamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.eljame.com/mktba/play.php?catsmktba=160#UP
  • Imechapishwa: 22/04/2015