Moja ya mitihani mikubwa ambayo imewapata Waislamu leo na haya makundi al-Ikhwaan al-Muslimuun na mielekeo yake mitatu:

1 – Bannaaiyyah, baada ya muasisi Hasan al-Bannaa.

2 – Qutbiyyah, baada ya Sayyid Qutwub .

3 – Suruuriyyah, baada ya Muhammad Suruur.

Fikira zao zina uasi mkubwa; kutoka katika Sunnah na kutoka katika mkusanyiko (al-Jamaa´ah).

Kuhusiana na Sunnah, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema wakati alipoulizwa kuhusu kundi lililookoka:

“Ni lile linalofuata yale ninayofuata mimi hivi leo na Maswahabah zangu.” (at-Tirmidhiy ( 2641 )

Ameamrisha kufuata njia yake na njia ya Makhaliyfah wake na kusema:

“Shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhaliyfah wangu waongofu baada yangu. Shikamaneni nazo bara bara na ziumeni kwa magego yenu. Jiepusheni na mambo ya kuzua. Hakika kila kitachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.” at-Tirmidhiy (2676)

Wazi wazi kabisa wameacha Sunnah hii katika vitabu vyao, kazi zao na makala zao ambavyo vina upotevu mwingi kutoka katika Sunnah, kuwakemea wanaoshikamana na mfumo wa Salaf, Bid´ah na kuwasifia Ahl-ul-Bid´ah.

Ama kuhusiana na mkusanyiko, wao wanaonelea kuwa haifai kumtii mtawala wa Kiislamu na kwamba inatakiwa kufanya uasi dhidi yake. Wanawachochea ´Awwaam waleo na wale wasiokuwa na elimu dhidi yake katika nchi zote ambapo wana ulinganio. Maandiko ambayo yanaamrisha kumtii mtawala, kulazimiana na kushikamana na njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake wanayafasiri kimakosa na wanadai kwamba Salaf walikuwa na tafsiri mbili kwa hayo yote:

1 – Mkusanyiko unakuwa tu kwa yule kiongoze ambye watu wamekubalina naye, yaani kiongozi ambaye anaenda sambamba na Qu-aan na Sunnah. Hii ndio maana halisi ya mkusanyiko, wanaita pia kuwa ni siasa.

2 – Mkusanyiko ni wale wanaofuata yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na Maswahabah zake, pasina kujali kama atakuwepo mtawala au hakuna. Hii ndio maana ya kielimu kuhusiana na mkusanyiko, inaitwa pia siasa ya kiroho.[1]

Kwa ajili hiyo ndio maana wanasema kuwa Waislamu hawana makusanyiko wowote wala kiongozi kutokana na tafsiri ya kijumla pamoja na kwamba wao wanajua kuwa Saudi Arabia, inayotekeleza Shari’ah, [ni nchi] ambayo ipo na kadhalika nchi zingine pia za Kiislamu ambazo watawala wake ni vigumu kuwafanyia Takfiyr. Lakini kwa sababu ya kutaka kuendesha na kudanganya na kuepuka kizuizi hiki, wanayageuza maandiko ili waweze wafikia kwamba nchi pekee inayojulikana ni ya Ukhalifa wa kifalme au nchi ambayo inatangaza kuwa viongozi wote ni waislamu. Kwa ajili hiyo ndio maana wakatumbukia katika upotevu mwingine ikiwa ni pamoka na tafsiri za kimakosa za maandiko ya Kishari’ah. Jengine ni kwamba wao wanapinga maafikiano ya waislamu. Jengine pia ni kwamba wanapinga ukweli wa kihakika. Baadhi yao wana papara ya hali ya juu kwa kiasi ya kwamba wanamfanyia Takfiyr mtawala wa nchi hii – Saudi Arabia – na nchi nyinginezo. Baadhi ya hawa ni Abu Qataadah, Abu Muhammad al-Maqdisiy, Muhammad Suruur na wengineo.

(1) ath-Thawaabit wal-Mughayyiraat,uk. 19, cha Salaah as-Saawiy.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Saalim as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fikr-ut-Takfiyr, uk. 92-94
  • Imechapishwa: 22/04/2015