Jipime maarifa yako kuhusu twahara na swalah

Chemsha Bongo ya twahara na swalah 04

15:00

Unachenguka wudhuu wa ambaye amekula nyamafu?

Kuanza kwa Ramadhaan kunathibiti kwa ushahidi wa watu wangapi waadilifu?

Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya imamu unayemjua anapiga rimli (mganga)?

Lini unamalizika muda wa Dhuhaa?

Nani anayetangulizwa mbele kuwa imamu kati ya aliyehifadhi mvuta sigara na anavaa isbaal na mwingine amehifadhi kiasi lakini anafuata Sunnah?

Swalah ya Dhuhr ina Sunnah (Rawaatib) ngapi kabla na baada yake?

Kila ambaye inafaa kukusanya swalah anatakiwa vilevile kufupisha swalah?

Ni ipi hukumu ya ambaye amekumbuka swalah aliyokosa baada ya siku 2?

Ni sahihi msemo unaosema kwamba Sutrah ya imamu ni Sutrah ya maamuma?

Swalah ni nguzo ya ngapi katika zile nguzo tano za Uislamu?

Ni lini mtoto huanza kuamrishwa kuswali?

Vipi kuswali kitambo kidogo kabla ya kuingia wakati wa swalah?

Kuna udhuru gani wa mwanaume kuacha kuswali mkusanyiko msikitini?

Je, swalah inasihi nyuma ya imamu mnyoa ndevu?

Ni lini inaswaliwa Sunnah (Raatibah) ya kabla ya Fajr?

Je, ipi hukumu ya kutaja jina la Allaah kabla ya kuanza kutawadha?

Ni lini mwisho wa wakati wa swalah ya Ishaa?

Lini unaanza wakati wa kuswali Dhuhaa na ina Rakah ngapi?

Ni ipi katika hizi ni swalah ya kuomuomba Allaah mwongozo (ushauri) wakati unaposhindwa kuamua moja katika mambo mawili?

Ni ipi hukumu ya kufanya manuizi kwa kutamka kwa sauti kavla ya swalah?

Ni ipi katika hizi ni swalah ya kuomba kuteremshiwa mvua?

Ni kipi katika haya ni mojawapo ya nguzo za swalah?