Swali: Mwanamke anatumia dawa ya kichwa na ndani yake kuna asilimia kidogo ya poimbe. Je, inajuzu?

Jibu: Ikiwa ndani kuna kilevi haifai kuitumia kama dawa:

“Kingi kinacholevya basi kidogo chake pia ni haramu.”

Swali: Vipi ikiwa dawa hiyo inatumiwa nje ya mwili na hailiwi wala kunywewa?

Jibu: Haijalishi kitu. Udhahiri wa Sunnah ni kwamba inakatazwa. Kwa sababu kupatikana kwake ni njia inayopelekea kunywewa na kuliwa.

Swali: Vipi yale yanayonasibishwa kwa Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) kwamba amejuzisha hilo?

Jibu: Sidhihirikiwi na kitu. Kinacholevya hakitumiwi. Ambacho kina kileo hakitumiwi. Ni mamoja kinatumiwa kama mafuta, kichwani wala dawa:

“Enyi waja wa Allaah, jitibisheni! Na wala msijitibishe kwa haramu.”

Swali: Hukumu ni hiyohiyo juu ya manukato yaliyo na asilimia kidogo ya pombe? an

Jibu: Ndio. Tumefikiwa na khabari kwamba manukato yanayoitwa ´cologne` ndani yake kuna pombe na kileo.

Swali: Baadhi yake ni asilimia ndogo?

Jibu: Kukipatikana ndani yake kileo yaepukwe. Yasitumiwe ikitambulika kuwa ndani kuna kileo kinachotumiwa na watu.

Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kila kinacholevya ni haramu.”

Vipi kukitumia kwa njia ya kujitibisha?

Jibu: Kila kileo ni pombe na kila kileo ni haramu. Kingi kinacholevya basi kidogo chake pia ni haramu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23624/حكم-الكحول-في-الطيب-والدواء
  • Imechapishwa: 05/03/2024