Kutema mate upande wa Qiblah ndani na nje ya swalah

Swali: Wakati mwingine mdomoni kunabaki vipande vidogo vya Siwaak na akavitema mbele yake. Je, imekatazwa?

Jibu: Allaah ndiye anayejua zaidi… kutema upande wa kushoto ndio bora kwa hali yoyote. Hadiyth zilizopokelewa ni kuhusu ndani ya swalah. Hata hivyo aweke upande wake wa kushotoni. Baadhi ya mapokezi yanafasiri mengine. Bora na salama zaidi ni akiviweka upande wake wa kushotoni.

Swali: Mtoa maelezo ametaja kutoka kwa Ibn Khuzaymah kwamba mwenye kutema upande wa Qiblah basi atakuja siku ya Qiyaamah akiwa na mate yake machoni mwake. Je, hili ni kuhusu ndani ya swalah?

Jibu: Inawezekana ikawa hivo. Hilo linatilia nguvu kwamba bora ni yeye ateme upande wa kushotoni mwake. Kuhusu ndani ya swalah inakuwa ni lazima kufanya hivo, kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… asiteme… “

Haya ni makatazo. Msingi ni kwamba makatazo yanapelekea katika uharamu. Asiteme mbele yake ndani ya swalah kabisa; si katika swalah ya inayopendeza, swalah ya faradhi, msikitini wala maeneo mengine. Inapokuja nje ya swalah ni suala linalohitaji kuangaliwa vyema, ingawa ni jambo lenye wasaa. Lakini kamili na salama zaidi ni ateme upande wa kushotoni mwake hata akiwa nje ya swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23604/حكم-التفل-تجاه-القبلة-في-الصلاة-وغيرها
  • Imechapishwa: 05/03/2024