Jengine ni kwamba napenda kuzindua kitu kinachotumiwa na watu wengi pasi na wao kujua kuwa ndani yake mna kileo. Mfano wa bia. Hata kama wanasema kuwa haina kileo hawatakiwi kusadikishwa. Mfano mwingine ni matibabu yenye kileo. Nimepewa khabari kuwa dawa nyingi za kunywa zina kileo. Vivyo hivyo manukato yenye kileo, kwa sababu mwenye kujitia manukato amebaba na kununua pombe. Imekwishatangulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah ameilaani pombe na mwenye kuinywa, mwenye kuihudumia, mwenye kuiuza, mwenye kuinunua, mwenye kuitengeneza, mwenye kutengenezewa, mwenye kuoda na kula thamani yake.”[1]

Ikiwa pombe ni haramu basi ni haramu vilevile kuiuza.

[1] Abu Daawuud na al-Haakim. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (5091).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 274
  • Imechapishwa: 15/04/2025