Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا الرِّبَا أَضْعَافًا مُّضَاعَفَةً ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
”Enyi walioamini! Msile ribaa mkizidisha maradufu juu ya maradufu; na mcheni Allaah mpate kufaulu.”[1]
Aayah hii inakataza kula ribaa na kwamba ni moja katika sababu za kufaulu. Kuacha kula ribaa ni moja ya sababu ya kupata nusura dhidi ya maadui, sababu ya kupata uchumi mzuri na kufanikiwa kwa mikataba ya kifedha, sababu ya kujitenga mbali na mitihani. Kwa sababu Allaah amesema:
لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
”… mpate kufaulu.”
Ni mafanikio ambayo hayakufungamanishwa duniani na Aakhirah.
Isitoshe ribaa ni katika madhambi makubwa. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jiepusheni na dhambi saba zenye kuangamiza.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni yepi hayo?” Akasema: “Ni kumshirikisha Allaah, uchawi, kuiua nafsi ambayo Allaah kaiharamisha kuuliwa isipokuwa kwa haki, kula ribaa, kula mali ya mayatima, kukimbia siku ya vita na kuwazulia uongo wa kuzini wanawake waumini waliohifadhika.”[2]
[1] 03:130
[2] al-Bukhaariy (2767) na Muslim (89).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 276-277
- Imechapishwa: 15/04/2025
Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا الرِّبَا أَضْعَافًا مُّضَاعَفَةً ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
”Enyi walioamini! Msile ribaa mkizidisha maradufu juu ya maradufu; na mcheni Allaah mpate kufaulu.”[1]
Aayah hii inakataza kula ribaa na kwamba ni moja katika sababu za kufaulu. Kuacha kula ribaa ni moja ya sababu ya kupata nusura dhidi ya maadui, sababu ya kupata uchumi mzuri na kufanikiwa kwa mikataba ya kifedha, sababu ya kujitenga mbali na mitihani. Kwa sababu Allaah amesema:
لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
”… mpate kufaulu.”
Ni mafanikio ambayo hayakufungamanishwa duniani na Aakhirah.
Isitoshe ribaa ni katika madhambi makubwa. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jiepusheni na dhambi saba zenye kuangamiza.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni yepi hayo?” Akasema: “Ni kumshirikisha Allaah, uchawi, kuiua nafsi ambayo Allaah kaiharamisha kuuliwa isipokuwa kwa haki, kula ribaa, kula mali ya mayatima, kukimbia siku ya vita na kuwazulia uongo wa kuzini wanawake waumini waliohifadhika.”[2]
[1] 03:130
[2] al-Bukhaariy (2767) na Muslim (89).
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 276-277
Imechapishwa: 15/04/2025
https://firqatunnajia.com/hakuna-mafanikio-ya-ribaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)