Swali: Leo picha zimeenea. Je, ni haramu kuchukua picha kwa camera ya simu?

Jibu: Haijuzu kuchukua picha kwa kutumia njia yoyote ile. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mapicha na amewalaani watengeneza picha sawa kwa njia yoyote ile. Kinachozingatiwa sio ile njia inayotumiwa. Kinachozingatiwa ni kule kupatikana kwa picha. Haijuzu. Isipokuwa kama kuna dharurah kwa mfano kitambulisho, pasipoti na leseni. Haya ni dharurah na hayana neno. Ama mapicha kwa njia ya sanaa au mengineyo, haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2025-12-1435.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015