Pete kwa wanaume ni Sunnah au imeruhusiwa tu?

Swali: Kuvaa pete ni Sunnah au inaruhusu tu?

Jibu: Maoni ya karibu zaidi – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba ni Sunnah kwa watawala. Kuhusu watu wa kawaida tunafupizika kusema kwamba inaruhusu. Hata hivyo kwa watawala ni Sunnah. Mosi kwa ajili ya kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), pili ili waweze kupiga kwayo muhuri kwenye nyaraka mbalimbali. Imepokelewa kwenye upokezi wa Abu Daawuud kupitia kwa Abu Rihaanah makatazo ya kuvaa pete isipokuwa tu kwa watawala. Hata hivyo kuna kasoro katika kusihi kwake. Lakini inafasiriwa namna hii endapo imesihi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24433/حكم-اتخاذ-الخاتم
  • Imechapishwa: 25/10/2024