Hoja ni kwa yale yaliyopokelewa, na si kwa kitendo cha Ibn ´Umar

Swali: Hadiyth ya Ibn ´Umar inayosema kupunguza ndevu kiasi cha ngumi?

Jibu: Hayo ni katika matendo yake, kufanya hivo ni kosa. Hayo ni katika matendo na ijtihaad yake. Sahihi ni kuziachia na asikate chochote. Haijalishi kitu hata zikizidi juu ya ngumi. Ijtihaad yake (Radhiya Allaahu ´anh) inapingana na yale yaliyopokelewa. Kwa hivyo mtu asikate kilichozidi ngumu… Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuziachia na kuzifuga. Kuhusu kitendo cha Ibn ´Umar katika hijjah ni kutokana na ijtihaad yake. Maimamu wamemtia (Radhiya Allaahu ´anh) kwenye makosa katika jambo hili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24429/حكم-اخذ-قدر-القبضة-من-اللحية
  • Imechapishwa: 10/10/2024