Mswaliji ametengana na imamu ambaye ameswali Rak´ah pungufu

Swali: Kuna mtu ameingia na akamkuta imamu ameshaswali Rak´ah moja ya Maghrib ambapo akaswali naye Rak´ah moja. Wakati imamu aliposwali Rak´ah ya pili akasahau na akatoa salamu katika Rak´ah ya pili. Mtu huyu ambaye amekuja kuchelewa akasimama ili kuswali kile kilichompita. Imamu akakumbushwa ambapo akasimama kuleta kile alichokisahau. Ni kipi kilichosuniwa kufanya kwa yule ambaye amekwishatengana na imamu?

Jibu: Arudi pamoja na imamu na akamilishe naye kisha alipe baada ya imamu kutoa salamu. Arudi pamoja na imamu na akamilishe Rak´ah ya pili kisha alipe Rak´ah ya tatu. Isipokuwa ikiwa ameshatengana naye, katika hali hiyo ameshatekeleza kile kinachompasa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24435/حكم-مسبوق-فارق-الامام-ثم-عاد-الامام-لسهو
  • Imechapishwa: 11/10/2024