Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن ابن مسعود رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (الجَنَّةُ أَقْرَبُ إِلَى أَحَدِكُمْ مِنْ شِرَاكِ نَعْلِهِ، وَالنَّارُ مِثلُ ذلِكَ). رواه البخاري

105 – Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pepo iko karibu zaidi na mmoja wenu kuliko kamba za viatu vyake. Na Moto ni vivyo hivyo.”

Ameipokea al-Bukhaariy

Mtu anaweza kutamka neno moja ambalo likamridhisha Allaah (´Azza wa Jall), na asilitilie uzito, na likamwingiza katika Pepo yenye neema. Pamoja na hivyo Hadiyth hii ni muhimu zaidi kuliko hivo. Hakika kule kukithirisha zaidi ´ibaadah na kujiepusha na mambo ya haramu ni miongoni mwa sababu za kuingia Peponi. Haya ni mepesi kwa yule ambaye amewepesishiwa na Allaah (´Azza wa Jall).

Utaona muumini ambaye Allaah amemkunjulia kifua chake kwa Uislamu anaswali kwa raha, utulivu, moyo mkunjufu na ni mwenye kupenda swalah. Kadhalika anatoa zakaah, anafunga, anahiji na kufanya mambo mengine ya kheri. Mtu huyu ´ibaadah inamkuwia nyepesi kwake na sahali. Vilevile utamuona ni mwenye kujitenga na yale ambayo Allaah amemharamishia, katika mananeo na matendo, na yanamkuwia mepesi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/99-100)
  • Imechapishwa: 01/01/2024