Pale ambapo mlemavu anatambulika kwa upungufu wake

Swali: Baadhi ya watu wanapoambiwa wasimtie aibu fulani wanajibu kwamba watu hawamtambui isipokuwa kwa kumtambulisha kwa aibu yake.

Jibu: Hapa ni pale ambapo anatambulika kwa njia hiyo. Katika hali hiyo haidhuru. Ni kama mfano wa inaposemwa al-A´mash (mgonjwa wa macho) na al-A´raj (kiguru). Kuna wanafunzi wa Maswahabah waliokuwa wakiitwa hivo. Wote hawa ni wanafunzi wa Maswahabah na wapokezi wanaoaminika. Walikuwa wakitambulika kwa majina hayo. Vivyo hivyo al-A´war (chongo) alitambulika kwa jina hilo. Kwa hivyo haiwi usengenyi muda wa kuwa ndio jina analotambulika kwalo. Katika hali hiyo haiwi usengenyi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23437/حكم-مناداة-الشخص-بعيب-لا-يعرف-الا-به
  • Imechapishwa: 20/01/2024