Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
164 –
عَنْهُ أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم أَمَرَ بِلَعْقِ الأَصَابِعِ وَالصَّحْفَةِ، وَقَالَ: (إنَّكُمْ لا تَدْرونَ في أَيِّها البَرَكَةُ). رواه مسلم
Jaabir bin ´Abdilaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuramba vidole na sahani na kusema “Hakika nyinyi hamjui baraka iko wapi”.”[1]
Katika upokezi mwingine imekuja:
إِذَا وَقَعَتْ لُقْمَةُ أَحَدِكُمْ فَلْيَأخُذْهَا، فَليُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذىً، وَلْيَأكُلْهَا وَلا يَدَعْهَا لِلشَّيطَانِ، وَلا يَمْسَحْ يَدَهُ بالمنْدِيلِ حَتَّى يَلْعَقَ أصَابعَهُ فَإِنَّهُ لا يَدْرِي في أيِّ طَعَامِهِ البَرَكَةُ
“Mmoja wenu anapoponyokwa na chakula aokote na aondoshe palipopatwa na uchafu na halafu alile na asimwachie nalo shaytwaan. Asipanguse mkono wake na taulo mpaka arambe kwanza vidole vyake. Kwani hakika hajui ni wapi baraka ilipo.”[2]
Katika upokezi mwingine imekuja:
إنَّ الشَّيطَانَ يَحْضُرُ أَحَدَكُمْ عِنْدَ كُلِّ شَيءٍ مِنْ شَأنِهِ، حَتَّى يَحْضُرَهُ عِنْدَ طَعَامِهِ، فَإذَ سَقَطَتْ مِنْ أَحَدِكُمْ اللُّقْمَةُ فَليُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذَىً، فَلْيَأكُلْهَا وَلا يَدَعْهَا لِلشَّيطَانِ
“Hakika shaytwaan humwendea mmoja wenu katika kila jambo miongoni mwa mambo yake mpaka wakati wa kula. Mmoja wenu anapoponyokwa na chakula aondoshe palipopatwa na uchafu kisha alile na asimwachie nalo shaytwaan.”[3]
Mtu akifanya haya kwa minajili ya kujisalimisha na maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kunyenyekea kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kumnyima shaytwaan asile, kunapatikana kwa kufanya hivi faida tatu:
1 – Anakuwa ametekeleza maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
2 – Unyenyekevu.
3 – Kumnyima shaytwaan chakula.
Kuna faida hizi tatu.
Pamoja na hivyo watu wengi wanapoponyokwa na chakula tena mahala pasafi, anakiacha. Hili linaenda kinyume na Sunnah.
[1]Muslim (2033).
[2]Muslim (2033)
[3]Muslim (2033).
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/300)
- Imechapishwa: 29/12/2024

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/300)
Imechapishwa: 29/12/2024
https://firqatunnajia.com/okota-chakula-kipanguse-na-ukile-kinapoanguka/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)