20 – Khaalid bin Makhlad ametuhadithia: Sulaymaan bin Bilaal ametuhadithia: Suhayl amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Ameangamia! Ameangamia! Ameangamia!” Wakasema: ”Ni nani, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: ”Ni kwa yule atakayekutana na wazazi wake wawili katika utuuzima wao, au mmoja wao, kisha akaingia Motoni.”
21 – Abuun-Nu´maan Muhammad bin al-Fadhwl ametuhadithia: Abu ´Awaanah ametuhadithia, kutoka kwa Suhayl bin Abiy Swaalih, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Ameangamia! Ameangamia! Ameangamia yule atakayekutana na wazazi wake wawili katika utuuzima wao, au mmoja wao, kisha akaingia Motoni.” Au alisema ”… kisha asiingie Peponi.”
22 – Musaddad ametuhadithia: Bishr bin al-Mufadhdhwal ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Ishaaq ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd al-Maqburiy, kutoka kwa Abu Hurayrah,kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Maangamivu ni kwa yule ambaye nitatajwa mbele yake na asiniswalie. Maangamivu ni kwa yule ambaye atakutana na wazazi wake wawili katika utuuzima wao, au mmoja wao, na wasimwingize Peponi. Maangamivu ni kwa yule ambaye atakutana na Ramadhaan kisha ikamalizika kabla ya yeye kusamehewa.”
23 – Ibn Abiy Uways ametuhadithia: Kaka yangu amenihadithia, kutoka kwa Sulaymaan bin Bilaal, kutoka kwa Muhammad bin Hilaal, kutoka kwa Sa´d bin Ishaaq bin Ka´b bin ´Ujrah as-Sulamiy, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kwamba Ka´b bin ´Ujrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hudhurieni kwenye mimbari!” ambapo tukahudhuria. Alipopanda daraja ya kwanza akasema ”Aamiyn.” Alipopanda daraja ya pili akasema ”Aamiyn.” Alipopanda daraja ya tatu akasema ”Aamiyn.” Alipotua tukasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Leo tumekusikia ukisema kitu ambacho hatujapatapo kukusikia ukikisema.” Akasema: “Mmesikia?” Tukasema: “Ndio.” Akasema: ”Jibriyl amejidhihirisha na kusema: ”Atokomee mbali yule ambaye itamfikia Ramadhaan na asisamehewe.” Nikasema: ”Aamiyn.” Nilipopanda daraja ya pili akasema: ”Atokomee mbali yule ambaye jina lako litatajwa mbele yake na asikuswalie.” Nikasema: ”Aamiyn.” Nilipopanda daraja ya tatu akasema: ”Atokomee mbali yule ambaye atadiriki uzee wa wazazi wake wawili, au uzee wa mmoja katika wao, na asiingie Peponi kwa ajili yao.” Nikasema: “Aamiyn”.”[1]
24 – Abu Nu´aym ametuhadithia: Salamah bin Wardaan ametuhadithia: Nimemsikia Anas akisema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipanda juu ya mimbari na kusema katika ile daraja ya kwanza: ”Aamiyn.” Kisha akapanda daraja ya pili na kusema: ”Aamiyn.” Kisha akapanda daraja ya tatu na kusema: ”Aamiyn.” Alipofika juu yake akaketi. Maswahabah wake wakasema: ”Ni kwa nini umesema ”Aamiyn”, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: ”Jibriyl (´alayhis-Salaam) amenijilia na kusema: ”Maangamivu ni kwa yule ambaye utatajwa mbele yake na asikuswalie.” Nikasema: ”Aamiyn.” Kisha akasema: ”Maangamivu ni kwa yule ambaye atakutana na wazazi wake wawili katika utuuzima wao, au mmoja wao, na wasimwingize Peponi.” Nikasema: ”Aamiyn”.”
[1] Swahiyh kupitia zengine.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 119-122
- Imechapishwa: 29/12/2024

Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 119-122
Imechapishwa: 29/12/2024
https://firqatunnajia.com/10-maangamivu-ni-kwa-yule-ambaye-atakutana-na-wazazi-wawili-na-wasimwingize-peponi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)