09. Kuwaasi wazazi wawili ni katika madhambi makubwa

19 – Musaddad ametuhadithia: Bishr bin al-Mufadhdhawl ametuhadithia: al-Jurayriy amenihadithia, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakrah, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nisikuelezeni madhambi makubwa kabisa?” Akakariri hivo mara tatu. Wakasema: ”Ndio, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: ”Kumshirikisha Allaah na kuwaasi wazazi wawili.” Akaketi na alikuwa ameegemea na kusema: ”Ushahidi wa uwongo.” Akaendelea kuyakariri mpaka tukatamani laiti angenyamaza.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 118
  • Imechapishwa: 29/12/2024