Wanachuoni wametofautiana juu ya kuthiriwa:

1 – Kuna ambao wamesema ni wajibu kwa wavulana na wasichana. Wamesema ni wajibu kumtahiri msichana kama jinsi ni wajibu vilevile kumtahiri mvulana.

2 – Wengine wakasema kwamba kutahiriwa sio wajibu kwa wanaume wala wanawake. Wamesema kuwa kutahiriwa ni katika maumbile yaliyopendekezwa na sio ya wajibu.

3 – Wengine wakenda kati na kati kati ya kauli ya kwanza na ya pili na wakasema ni wajibu kwa wavulana na ni Sunnah kwa wanawake.

Hii ndio kauli ya kati na kati na adilifu. Ni wajibu kwa mwanaume kwa sababu kingozi hiki kikibaki kwa mwanaume kinakusanya mkojo na pengine mtu akadhurika. Sahihi ni kwamba kutahiriwa ni wajibu kwa watoto wa kiume na ni imependekezwa kwa watoto wa kike. Hii ndio kauli ilio kati na kati na bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/308-309)
  • Imechapishwa: 29/12/2024