Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ni kiburudisho kwenye macho ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah[1] na kipigo kikali kwa Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal.”

Bi maana masuala haya. Macho ya Ahl-us-Sunnah yanaburudika juu ya kumuona Allaah (´Azza wa Jall). Ni kipigo kwa wale wasioamini juu ya kuonekana kwa Allaah. Ni wenye kubabaika wakati wanapozipitia Aayah zinazozungumzia juu ya sifa – masikini hawa. Hili ni kwa sababu zinaenda kinyume na mfumo na I´tiqaad zao.

Mimi nilikaa kwenye kikao ambapo kunasomwa “Kitaab-ut-Tawhiyd” kutoka kwenye “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy. Ninaapa kwa yule ambaye hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, niliwaona ni kana kwamba wanapita kwenye njia ilio na khatari. Hawataki kujua maana ya maandiko haya. Wanasoma al-Bukhaariy kwa lengo la baraka. Hawataki kuelewa yaliyo ndani na wala hawataki kuchukua imani yenye kutolewa dalili na maandiko ya Mtume. Mu´tazilah, Jahmiyyah na Baatwiniyyah wengine. Wanababaika sana juu ya maandiko yanayozungumzia kumuona Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kiburudisho-kwenye-macho-ya-ahl-us-sunnah/

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 09-10
  • Imechapishwa: 26/08/2020